Zawadi za krismasi zimeanza kumfikia Floyd Mayweather hii imetoka kwa mashabiki wake

Siku zote unapoambiwa utaje list ya mastaa
waliowahi kutamba katika mchezo wa ngumi,
hauwezi ukaliacha jina la Floyd Mayweather mtu
wangu. Staa huyo ambaye ni bingwa wa
mchezo wa ngumi wa uzito wa kati amepokea
zawadi ya Tiger mwenye miezi miwili toka kwa
mashabiki wake kwa ajili ya Krismasi.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Mayweather
alipost picha akiwa na Tiger huyo, ambapo
kwenye caption ya picha hiyo, aliandika
kuwashukuru mashabiki wake wa jiji
la Moscow Urusi, kwa zawadi ya Krismas
waliyompatia pamoja na kuwaomba
wamchagulie jina la Tiger huyo.
“Napenda kuishukuru familia yangu pamoja na
mashabiki wangu toka Moscow kwa upendo
waliouonyesha wa kunizawadia Tiger kwa ajili ya
Krismasi, ni kitu kigeni toka kwangu, jina gani
nimpatie Tiger huyu wa kike mwenye miezi
miwili?”>>> Mayweather.
Msaidizi wa Mayweather ambaye anaitwa Marikit
Laurico akipiga picha na Tiger wa miezi miwili
aliyopewa zawadi Mayweather .
Floyd Mayweather ambaye hivi karibuni
alitangaza kustaafu mchezo wa ngumi baada ya
kupigana pambano lake la mwisho na bondia
Andre Berto na kumpiga, pambano ambalo
lilimfanya Floyd Mayweather kupambana jumla
ya mapambano 49 na kuendeleza rekodi yake ya
kushinda mapambano yote.

No comments

Powered by Blogger.