Hii ndio sababu pekee inayomfanya Alves kusema Ronaldo hakustahili kuwa katika tuzo za Ballon d’Or 2015 …
Headlines za wachezaji wanaowania tuzo ya
mchezaji bora wa Dunia kwa mwaka 2015
(Ballon d’Or) bado zinazidi kuchukua nafasi, kwa
sasa kila mmoja amekuwa akitaja mshindi wake
katika tuzo za Ballon d’Or 2015, baada ya
November 30 kutangazwa majina matatu
yaliofanikiwa kuingia fainali ya tuzo hizo
zitakazotolewa Zurich Uswiss January 11 2016.
Baada ya mashabiki wengi wa soka kuongea au
kutaja kila mchezaji wake anayedhania kuwa
anastahili kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or
kati ya Lionel Messi , Neymar na Cristiano
Ronaldo , December 4 imekuwa ni siku ya beki
wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania na timu
ya taifa ya Brazil Daniel Alves kuzungumza au
kutaja mtu anayestahili kushinda tuzo hiyo.
Alves hakuishia kumtaji Lionel Messi pekee
kuwa ndio atakuwa mshindi January 11 2016
kati ya majina ya wachezaji hao watatu
waliofanikiwa kuingia katika kuwania tuzo hizo,
bali amesema Cristiano Ronaldo hakustahili
kuwa nominated katika Top 3 hiyo, kwani
mchezaji bora wa Dunia sio kufnga magoli
pekee.
“Messi atashinda kutokana na mchango au
ushawishi wake katika mchezo, nafikiria Neymar
kwa sasa ndio wa pili kwa ubora baada ya Lionel
Messi , Cristiano Ronaldo hakustahili kuwa katika
tatu bora ya wanaowani tuzo ya Ballon d’Or kwani
hii haisishi ufungaji pekee” >>> Daniel Alves
No comments