Majibu ya Drake baada ya kusikia Adele angependa kufanya ‘remix’ ya Hotline Bling!
Baada ya Adele kuonyesha nia ya kutaka
kufanya remix ya Hotline Bling , kumekuwa na
minongono juu ya mtazamo wa Drake kwenye
ishu hiyo, watu wengi ikiwa mashabiki
wamekuwa wakitaka kujua nini kinaendelea
kichwani mwa Drake juu ya ombi la msanii huyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa etalk, Drizzy Drake
ameonyesha pia nia kubwa sana ya kufanya
remix hiyo na Adele muda wowote atakapokuwa
tayari… “Nitafanya kitu chochote na Adele, hata
akitaka niende kwake kumsaidia kufua nitaenda,
nipo tayari hata sasa hivi “, alisema rapper huyo.
Drake & Adele.
Alipoulizwa kama atakuwa tayari pia
kumfundisha Adele style za uchezaji wa ngoma
hiyo, Drake aliuambia mtandao wa etalk kuwa
angependa kufanya hiyo lakini hatojua pa
kuanzia kwani style zote alizokuwa anazicheza
zilikuwa kama freestyle na sio kwamba alifanya
mazoezi popote…
>>> “Sikupanga kucheza vile, zile style zilikuja
natural, na nia ilikuwa kuwafanya watu wapate
muamko wa kujiamini pale wanapoisikia ngoma
yangu. Na kuona dunia nzima imeipokea kwa
namna walivyoipokea inanifurahisha sana. ” <<<
Drake.
No comments