Nimekutana na list ya wachezaji 10 wa kiislamu wanaolipwa mishahara mikubwa Uingereza
Mchezo wa soka ni mchezo ambao unalipa
kwani siku hizi ni kawaida kuona wachezaji au vijana wenye umri mdogo
wakilipwa mishahara mikubwa kutokana na vipaji vyao, haijalishi umetokea
dini gani, kabila wala nchi gani, kinachotakiwa uwe na kipaji tu katika
soka, nimekutana na hii mtandaoni list ya wachezaji wakiislamu
wanaolipwa mishahara mikubwa Ligi Kuu Uingereza kwa mwaka 2015.
1- Yaya Toure wa Manchester City anaongoza kwa kulipwa mkwanja mwingi zaidi kuliko mchezaji yeyote wa kiislamu Uingereza, analipwa pound 180,000 kwa wiki.
2- Mesut Ozil kutoka klabu ya Arsenal anafuatia kwa kuingiza pound 140000 kwa wiki hii inatokana na uwezo wake mkubwa uwanjani.
3- Marouane Fellaini wa Man United inawezekana usiamini kuwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaoamini dini ya kiislamu kutokana na nchi nyingi za Ulaya uaminika waislamu kuwa wachache yeye anavuta pound 100000 kwa wiki.
4- Samir Nasri huyu ana asili yake kutokea Afrika licha ya kuwa ni mfaransa kwa sasa lakini asili yake haishangazi kusikia ni muislamu kwani ana asili ya Argeria akiwa na Man City huwa anavuna pound 90000.
5- Bacary Sagna huenda ukawa unashangazwa na muonekano wake kichwani na kuhisi huyu sio muislamu ila ni beki mahiri wa Man City analipwa pound 70000 kwa wiki.
6- Mamadou Sakho yupo sawa na mfaransa mwenzake Bacary Sagna kwani na yeye analipwa pound 70000 kwa wiki.
7- Kolo Toure mdogo wake wa damu Yaya Toure anaongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu zaidi ya kaka yake Kolo, kwa sasa Kolo Toure analipwa pound 65000 kwa wiki.
8- Adnan Januzaj wa Man United anaondoka na kiasi cha pound 60000 kwa wiki ila yupo sawa na Kurt Zouma wa Chelsea.
9- Kurt Zouma sio maarufu sana kutokana na nafasi yake kuwa finyu ya kucheza Chelsea kitu kinachopelekea kukaa benchi mara kwa mara kwa nyota huyo, analipwa pound 60000 kwa wiki.
10- Papiss Cisse mkali mwingine kutokea Senegal anayekipiga katika klabu ya Newcastle United ndio anaitimisha top 10 ya mastaa hawa kwa kulipwa pound 58000 kwa wiki.
No comments