Mimba ya Jokate Yazua Balaa

Kwani kimenuka? Siku chache baada ya
kubumburuka kwa habari ya kunasa mimba
ikimhusisha ‘mtoto mzuri’ Bongo, Jokate
Mwegelo ‘Kidoti’ huku mhusika mkuu akitajwa
kuwa ni msanii nguli wa Bongo Fleva, Ali Kiba,
ishu hiyo imezua balaa kufuatia familia ya
mrembo huyo kushtushwa na hali hiyo, Ijumaa
Wikienda limenyetishiwa.
TWENDE OYSTERBAY
Mwishoni kwa wiki iliyopita, ‘kijumbe’ wa gazeti
hili alitua getini nyumbani kwa akina Jokate,
Oysterbay jijini Dar kwa lengo la kutaka kujua
nini kinaendelea juu ya binti yao kunasa mimba
nje ya ndoa ilihali familia hiyo inasifika kwa
misingi bora na maadili ya kidini.
Gazeti hili lilipotia timu nyumbani hapo,
lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa
wanafamilia hiyo aliyekuwa nje akifanya usafi
ambaye bila simile ‘alifunua kinywa’ na kuweka
hadharani mambo mazito.
GAZETI LA IJUMAA LAIBUA MAMBO
Kama anayeogopa jambo fulani, memba huyo wa
familia ya Jokate alisema kuwa, mrembo huyo
alikuwa akifanya siri kubwa juu ya ujauzito wake
huo, lakini baada ya gazeti pacha la hili, Ijumaa,
kuibua habari hiyo, familia hiyo, hususan mama
yake mzazi (jina lipo), alizua utata mkubwa kwa
binti huyo na kwamba alishtushwa na hali hiyo
na kumlazimu kumkalisha ‘kitako’ Jokate ampe
ukweli.
“Jokate alikuwa akifanya siri sana, lakini ninyi
mlipoandika habari hiyo, hapakutosha, mama
yake alimuitisha kikao na baadhi ya ndugu
wengine, lakini Jokate hakutaka kuweka wazi juu
ya hali hiyo.
“Ninavyosikia, kuna uwezekano mkubwa wa
Jokate kuhama hapa nyumbani akajitegemee ili
kuififisha aibu hii kwani familia inadai amewatia
aibu kwa kitendo chake cha kubeba mimba nje
ya ndoa,” alidai mhusika huyo.
JOKATE ATOWEKA
Mnyetishaji wetu huyo aliendelea kudai kwamba,
baada ya kuona anabanwa, alitoweka nyumbani
hapo kwa siku mbili kabla ya kurejea na
kuondoka kisha kurejea tena.
Kama kawaida ya gazeti hili kujiridhisha kwa kila
habari kabla ya kuichapisha na kuwapelekea
wasomaji wake, ‘kiranja mkuu’ wa dawati la
Ijumaa Wikienda, mashine kubwa kwa habari za
ndani za mastaa wa Kibongo, alimtafuta mrembo
huyo kupitia simu ya mkononi na alipobaini kuwa
mpigaji ni mwandishi wetu alishindwa kusema
chochote zaidi ya kuiacha simu hewani na
baadaye kuikata.
ATUMIWA SMS
Hata hivyo, ili kujizolea ushahidi madhubuti,
mwanahabari wetu alimtumia ujumbe mfupi wa
maandishi (sms) na kumsomea madai hayo,
lakini hakujibu ujumbe huo licha ya simu ya
mwandishi wetu kuonesha kuwa ujumbe ulikuwa
umepokelewa (delivered).
KIBA KIMYAA
Pia, kwa upande wa Ali Kiba, simu yake
ilionekana kutokuwa hewani muda mwingi, lakini
mwandishi wetu alituma ujumbe wa kutaka
kusikia chochote kutoka kwake ili akiiwasha
simu akutane na ujumbe huo, lakini hadi gazeti
hili linaenda kuchapishwa, hakuwa amejibu
ujumbe huo achilia mbali kupiga simu hivyo
jitihada zinaendelea.
Hata hivyo, mashabiki wa mastaa hao
wameendelea kuwapongeza kwa namna
ambavyo wamekuwa wakioneshana mahaba na
kwamba suala la kupata mtoto ni jambo la heri
bila kujali wamefunga ndoa au la.

No comments

Powered by Blogger.