Riyama Kuwasaka Wanaomtumia
MSANII wa filamu Bongo Riyama Ally amesema baadhi ya wasanii
wanaomhitaji na kucheza nao filamu, huuza baadhi ya vipande vya filamu
anazocheza bila idhini yake, jambo alilodai hakubali kwani atawasaka na
kuwashikisha adabu.
Akizungumza na mwandishi wetu, alisema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia kava lenye picha yake kuuza filamu ambazo anakuwa hajacheza, isipokuwa zimechomekwa vipande alivyoigiza bila kukubaliana.
“Unakuta msanii ananifata nicheze filamu yake vipande sita, mwisho wa siku anatumia sini moja, halafu zingine anaziuza, wote wanauzia kava bila mimi kunufaika chochote, mfano kuna filamu inaitwa Nyota, Kigoma cha mtaa zote zijashiriki kabisa, nimeshaongea na Cosota wanisaidie katika hili, wote wanaofanya hivi nitawachukulia hatua kali za kisheria,”alisema.

No comments