Diamond, Kajala Mahaba Niue!
NI gumzo! Ubuyu motomoto ambao unasambaa
kwa kasi ya ajabu kama moto wa kifuu mjini
unadai kuwa, staa nambari moja Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwigizaji
Kajala Masanja wamedaiwa kuwa ni wapenzi na
sasa ni mahaba niue, Risasi Jumamosi
limesheheni full stori.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, uhusiano wa
Diamond na Kajala unadaiwa kuibuka ghafla
miezi kadhaa iliyopita lakini wamekuwa
wakifanya siri nzito kabla ya hivi karibuni
kukolea zaidi baada ya mpenzi wa Diamond,
Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kurudi nchini
mwake, Afrika Kusini ‘Sauz’.
“Walianza zile za kimjinimjini, wakawa
wanafanya yao kimyakimya tangu Zari akiwepo
lakini mahaba niue yamekuja kushamiri zaidi
baada ya Zari kutimkia zake Sauz,” kilisema
chanzo chetu.
MASTAA WAZUNGUMZIA
Mara baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu
huo, Risasi Jumamosi lilipenyezewa data kutoka
kwa mastaa tofauti ambao wanafahamu
uhusiano huo mpya ambao pia ulianza kusambaa
taratibu katika mitandao ya kijamii.
“Hivi kwani nyinyi hamjaipata habari hii?
Diamond amemnasa Kajala na mambo yao ni
bambam. Sema kiukweli Diamond ni msiri maana
unajua ana mambo mengi hivyo hapendi kabisa
hii ishu ijulikane,” alisema staa mmoja mkubwa
Bongo huku akiomba hifadhi ya jina.
Kama hiyo haitoshi, staa mwingine aliliambia
Risasi Jumamosi kuwa, dada wa Diamond, Esma
anaujua mchezo mzima na anatajwa
kuusambaza ubuyu huo kama malipo kwa Wema
(Sepetu) anayemtuhumu kumuibia bwana wake,
Petit Man.
“Esma ameamua kumwaga ugali maana Wema
na timu yake wamekuwa wakijitapa sana mjini
kwamba wamemnyakua mume wa Esma, Petit
Man. Na yeye anawaonesha kwamba kama ni
kuchukuliwa mbona hata Kajala amechukuliwa
na Diamond ambaye alikuwa mtu wa Wema
lakini wamekaa kimya,” alisema msanii huyo.
Jitihada za kumpata Esma ili aweze
kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba baada
ya simu yake ya mkononi kuita muda mrefu bila
kupokelewa.
MITANDAO YAZIDI KUKUZA JAMBO
Mpaka tunakwenda mitamboni, juzi, mitandao
mbalimbali hususan Instagram, wadau
walisambaza habari ya Kajala na Diamond huku
wakijaribu kumwambia Zari amtambue Kajala
kama mke mwenzie kwani ameshalala Madale,
nyumbani kwa Diamond.
“Zari mke mwenzio ni huyu hapa, anakusaidia.
Juzi amelala Madale na Diamond,” iliandikwa na
mdau mmoja wa Instangram.
ZARI ACHANGANYIKIWA
Chanzo kilichomwaga ubuyu huo kimeeleza
kuwa, taarifa za Kajala na Diamond zilipomfikia
Zari, alichanganyikiwa na kuanza kumcharukia
Diamond au baba Tiffah ambaye ilibidi atumie
nguvu ya ziada kumtuliza kwani bado wawili hao
wanaendeleza uhusiano wao huku wakijua Zari
hayupo Bongo.
“Zari alicharuka kwelikweli. Ilibidi Diamond
atumie nguvu ya ziada kumtuliza na bahati nzuri
mtoto wa kike ameelewa,” kilisema chanzo
chetu.
DIAMOND SASA
Alipotafutwa Diamond na kusomewa mashitaka
yake, mambo yalikuwa hivi:
Risasi Jumamosi: Kuna taarifa kwamba
unatembea na Kajala na sasa mahaba ni
motomoto, vipi kuna ukweli? Tena vyanzo
vingine vinadai kuna hadi picha za wewe na
Kajala mkiwa nyumbani kwako, unazungumziaje
hilo?
Diamond: Aaah! Siyo kweli mwanangu…picha
kweli mnazo? Picha gani…yaani kiaje?
Risasi Jumamosi: Inasemekana zipo ambazo
mpo nyumbani kwako, Madale.
Diamond: Aahaha! Aaah uongo mtupu siyo kweli.
Kama kuna picha kweli nitumieni basi.
KAJALA SASA
Alipopigiwa simu zaidi ya mara tano, Kajala
hakupokea. Risasi Jumamosi lilimtumia ujumbe
mfupi wa maneno (SMS) uliosomeka hivi:
“Habari, kuna ishu yako hapa Global Publishers,
inahusu madai ya wewe kutoka kimapenzi na
Diamond jambo ambalo linadaiwa kuleta
mtafaruku mkubwa kati yako na Zari. Pia hata
kwenye mitandao ya kijamii bila shaka umesikia,
naomba ufafanuzi wako tafadhari.”
Licha ya ujumbe huo kuonesha kumfikia, hadi
tunakwenda mitamboni, Kajala hakujibu
chochote.
KAMA NI HIVYO
Madai ya kuwepo kwa uhusiano huo yanaweza
kumweka Kajala katika mtazamo mwingine
kijamii, kwani miaka miwili nyuma alidaiwa
kutoka kimapenzi na mwanaume anayeitwa CK
ambaye hakuna shaka alikuwa mpenzi wa Wema
kabla ya kumwagana.
Hali hiyo ilizua mjadala, Kajala alibebeshwa
madai mazito kwamba alikuwa na uhusiano na
CK hata akiwa na Wema, ikitafsiriwa kwamba
alikuwa akimlia vyake mwenzake hali iliyozua
mgogoro wa wawili hao.
Diamond naye, amewahi kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na Wema, wakamwagana. Kitendo cha
kudaiwa kutoka na Kajala, kinazidi kumweka
mdada huyo katika mlolongo wa kudhaniwa
anamwandama Wema kwa vile kila alikopita,
yeye naye anapita!
No comments