Esha Buhet: Usanii Ushanibumia, Bora Niuze

MSANII wa filamu hapa Bongo, Esha Buhet
amefunguka kuwa kwa upande wa usanii anaona
umeshaenda kombo hivyo kuliko kukaa tu bora
afanye ujasiriamali wa kushona kofi a za nywele.
Akizungumzia maisha yake ya sasa baada ya
soko la filamu kuonekana kutolipa, Eshe alisema
kwa hali ya maisha ilivyo ujanja ni kutafuta kazi
mbadala ya kufanya na yeye ameamua kufanya
biashara hiyo ambayo angalau inamlipa.
“Mimi kwa kweli inawezekana labda usanii
niliingia kwa bahati mbaya sana naona ndiyo
maana hata mafanikio yake yalikuwa ni matatizo
sana, sasa nimeona kuliko kukaa barazani na
kupiga soga, bora nishone kofi a za nywele,
nipate vijihela ili maisha yaendelee, mjini hapa…
ohooo,” alisema Esha

No comments

Powered by Blogger.