Aunty Ezekiel Hataki Kufuatiliwa
STAA wa Bongo Movie ambaye kwa sasa ni
mama wa mtoto mmoja Aunty Ezekiel amesema
huwa anakerwa na watu ambao wanapenda
kufuatilia mahusiano yake na baba mtoto wake
Moses Iyobo, dansa wa Diamond Platinumz.
Aunty Ezekiel alisema, kuna baadhi ya watu
wanapenda kumfuatilia mahusiano yake na kudai
yeye amemzidi umri dansa huyo kitu ambacho
hapendezwi nacho.
Alisema huwa anawashangaa sana baadhi ya
watu ambao wanashidwa kufanya mambo yao na
kumjadili maisha yake.
“Jamani mimi sipendi maneno ya watu
wanaonijadili, nilivyokutana naye kwani hakujua
nimemzidi umri? Sipendi kufuatiliwa,” alilalama
Aunty. Alisema mambo yake na dansa huyo
wawaachie wao wenyewe, kwani wanajua kile
wanachofanya
No comments