Van Vicker kumfanyia sapraizi Wema
ZIKIWA zimesalia wiki kadhaa kabla ya kufanyika kwa sherehe ya bethidei ya muigizaji Wema Sepetu ‘Madam’, muigizaji wa Ghana, Van Vicker amesema amemuandalia zawadi ya ‘sapraizi’ mrembo huyo katika sherehe yake hiyo muhimu.
Akifunguka hayo kupitia katika akaunti yake ya Instagram, Van alimtakia Wema heri ya siku yake ya kuzaliwa kisha kumuahidi kwamba atakuwepo katika sherehe hiyo na ana sapraizi yake.
Akizungumzia sapraizi na salamu hizo kutoka kwa Van, Wema alisema anafurahi kuzisikia na kwamba sherehe hiyo itafana kama mwigizaji huyo wa Ghana akifanikiwa kuwepo.
Akizungumzia sapraizi na salamu hizo kutoka kwa Van, Wema alisema anafurahi kuzisikia na kwamba sherehe hiyo itafana kama mwigizaji huyo wa Ghana akifanikiwa kuwepo.
“Mimi naisubiri kwa hamu, kama nilivyowaambia bethidei yangu ilikuwa ifanyike Septemba 24 lakini niliisogeza mbele hadi Oktoba 28 ili nisherehekee ushindi wa CCM na bethidei kwa pamoja,” aliweka nukta Madam.
Chanzo:GPL
No comments