Haya ni maneno ya Idris Sultan kuhusu ujio wa TV Show yake mpya BET…!
Mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idris Sultan anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani… baada ya kuiwakilisha #255 vizuri kwenye shindano hilo kubwa la Africa, mafanikio mengi yamekuwa yakimfuata nyuma Idris Sultan!
Kama wewe ni miongoni wa watu wanaompenda na kumfuatilia Idris kwenye social networks basi hii good news ikufikie popote ulipo mtu wangu… Idris Sultan siku chache zilizopita alitudokeza kuhusu ujio wa TV Show yake mpya itakayo kuwa inaonyeshwa moja kwa moja kupitia channel ya BET pamoja na channel ya Vuzu za South Africa! Yote ikiwa ni sehemu ya kufanikisha ndoto zake kubwa za kwenda Hollywood, Marekani.
Staa huyo wa Tanzania ambae pia ni mchekeshaji mzuri sana alipata time ya kupiga stori na millardayo.com kuzungumzia nini kilimsukuma kuja na TV Show yake…
>>> “Kwanza
 niliwekwa kwenye auditions ambazo nilitakiwa kufanya ili kuingia kwenye
 Tv show ya ‘The Real Husbands of Hollywood’ show ambayo Kevin Hart 
yupo, na auditions zangu zilitakiwa zifanyike tarehe 26th April… sasa 
nikachelewa kuapply Visa ya kwenda USA kwasababu nilikuwa nafanya tours 
nyingi ndani ya Africa bado kitu kilichopeleka auditions zangu kuwa 
cancelled, chance hiyo ikanipita na hapo ndipo niliposukunwa sasa 
kuanzisha reality show yangu mwenyewe ili iwe rahisi kwa mimi kuonekana 
tena na kupata nafasi nyingine ya kuingia Hollywood…” <<< Idris Sultan.
Sikuishia hapo, nikamuuliza Idris reality show yake itakuwa inahusu nini na kama show hiyo haitaathiri ndoto zake za kuwa Mchekeshaji mkubwa duniani…
>>> “Reality
 show hainibadilishi mimi kama mimi kwasababu kwanza haina script, hiyo 
show itakuwa inaonyesha sana sana ninachokifanya, kwa mfano sasa hivi 
mnaona tu nafanya vitu tofauti lakini kupitia Reality Show yangu mtakuwa
 mnaviona ninavyovitimiza, nimevifanyaje, nimepitia nini, na pia muda 
gani niliwachekesha watu nusu kuzimia… vitu vyote hivi vitaonyeshwa, so 
kwa ufupi itakuwa inaonesha maisha yangu halisi haswa upande ambao 
hamuuoni nyinyi kila siku… na haitanipotezea muda bali itakuwa 
inaonyesha hustle yangu yote na vitu gani ambavyo navifanya mimi kama 
mimi, na comedy itakuwemo humo humo haitaathiri chochote, comedy zangu 
zote nitazifanyia humo humo!” <<< Idris Sultan.
Kama unakumbuka vizuri mtu wangu kuna kipindi Idris alianzisha kitu kinachoitwa ‘Hustle & Fame’ kwenye page yake ya Instagram, na inawezekana wengi wetu tumeona lakini hatujui ina maanisha nini… nikamuuliza Idris kama hili ndio jina la show yake mpya?, kwenye kupiga stori, staa huyo aliniambia haya…
Kwenye
 show mpya ya Idris Sultan tegemee kukutana na hawa watu mtu wangu, 
Samantha kutoka South Africa na  Luis Munana kutoka Namibia wote kutoka 
BBA 2014. 
>>> “Yea
 Reality Show itaitwa ‘Hustle & Fame’ na hilo jina hatukulipata 
kirahisi kwa sababu tulihangaika sana kama siku nne hivi tunatafuta tu 
jina, pia tulikuwa tunatafuta jina la show litakaloendana na uhalisia wa
 maisha yetu sisi ya kila siku tukiwa tayari maarufu lakini bado 
tunahangaika…” <<< Idris Sultan.
>>>
 “Tumeshafanya asilimia kubwa ya vitu tayari, kama episode 4 za mwanzo 
tayari tumeshashoot, tunasubiri tu kukamilisha vitu vidogo kama kusign 
mikataba na BET kama wakiipokea, hoteli tutakazotumia, makampuni ya 
ndege kwa ajili ya usafiri wa hapa na pale…” <<< Idris Sultan.
Reality TV Show ya Idris Sultan, ‘ Hustle & Fame’ itatumia lugha mbili, Kiingereza na Kiswahili na itaanza kuonyeshwa mwishoni wa mwaka huu wa 2015.


No comments