‘See You Again’ ya Wiz Khalifa ni video ya kwanza ya Hip-Hop kufikisha idadi hii ya watazamaji YouTUBE! + (Video)
Rapper maarufu kutoka Marekani, Wiz Khalifa anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani… miezi michache iliyopita msanii huyo aliachia single yake ya ‘See You Again’ wimbo uliyotumika kama official soundtrack kwenye movie ya Fast & Furious 7.
Licha ya wimbo huo kutumika kama soundtrack ya movie ya Fast & Furious 7, single hiyo pia ilikuwa ni wimbo wa kuienzi kumbukumbu ya muigizaji wa movie hiyo Paul Walker aliyefariki dunia kutokana na ajali ya gari November 30 mwaka 2013.. ukiacha hayo, kama wewe ni shabiki wa Wiz Khalifa na movie ya Fast & Furious 7 basi ikamate hii good news popote pale ulipo…
Video ya See You Again imefikisha idadi ya watazamaji Bilion 1 kwenye mtandao YouTUBE kuifanya single hiyo kuwa miongoni wa nyimbo kumi bora za YouTUBE kufikisha watazamaji bilioni 1 kufikia tarehe 7 mwezi October mwaka huu wa 2015!
Kitendo hiki kimemuweka Wiz Khalifa kwenye headlines kwa sababu yeye ndio msanii pekee wa Hip Hop ambae video yake imefanikiwa kufikisha idadi ya watazamaji Bilion1 kwenye mtandao wa YouTUBE na yote ikiwa ndani ya miezi 6 tu!
No comments