Uhusiano wa kwanza kabisa wa Kim Kardashian, alikua na miaka mingapi?...ona hapa!!

Unaweza ukadhani hakuna kingine kipya kuhusu maisha ya staa Kim Kardashian wa reality show ya ‘Keep Up with Kardashians’.
Upande wa maisha ya nyuma ya uhusiano wa Kim Kadarshian kabla ya kufunga ndoa na Kanye West, miongoni mwa wanaume aliowahi kuwa nao mapenzini ni pamoja na RJ, Reggie Bush, Kris Humphrie, Cristiano Ronaldo.
Lakini Kim Kardashian amesema kingine ambacho huenda hukuwahi kufahamu kuhusu uhusiano wake ya kwanza kabisa, aliingia mapenzini na mtoto wa kaka wa Michael Jackson aitwaye Tito Joe Jackson au TJ akiwa na miaka 14 tu.
kim na mama
Kim Kardashian akiwa na mama yake Kris Jenner
Katika kitabu cha kumbukumbu ya maisha yake kilichoandaliwa na Sean Smith kiliweka wazi uhusiano huo ambao hata hivyo haukudumu kwa muda mrefu na kuanza kutoka na RJ.

No comments

Powered by Blogger.