Mapenzi yake kwa Man United yafanya atumie zaidi ya saa 450 kutengeneza kitu hiki (+Pichaz)
Ushabiki wa soka kwa raia wa Uingereza unazidi kuchukua nafasi katika headlines za soka kila kukicha, August 30 2015 tuliona shabiki wa klabu ya West Ham United John High kuchora tattoo ya matokeo ya ushindi wa mechi dhidi ya Liverpool kwani kwa mujibu wa shabiki huyo anaweka kumbukumbu hiyo mwilini mwake kutokana na kuwa ni zaidi ya miaka 50 West Ham haijawahi kuifunga Liverpool.
August 7 shabiki mwingine wa klabu ya Manchester United Chris Scott anatajwa kutumia zaidi ya saa 450 katika kipindi cha miezi mitatu kutengeza mfano wa uwanja wa Old Trafford kama sehemu ya mapenzi yake kwa Man United . Chris Scott ametengeneza mfano wa uwanja wa Man United kama ulivyo hadi rangi.
Klabu ya Man United imekuwa ikiutumia uwanja wa Old Trafford kama uwanja wake wa nyumbani toka mwaka 1910, hata hivyo uwanja wa Old Trafford ndio uwanja wa pili kwa ukubwa nchini Uingereza baada ya uwanja wa Wembley ambao mara nyingi hutumiwa na timu ya taifa ya nchi hiyo.
No comments