Top 10 ya wasichana warembo katika mchezo wa tennis 2015 (+Pichaz)
Mchezo wa tennis ni moja kati ya michezo
 inayokuwa kwa kasi duniani kote, October 7 nakuletea Top 10 ya warembo 
wanaocheza mchezo wa tennis, list hii haitokani na umahiri wao wa 
kucheza tennis pekee bali hata fashion, muonekano wao. Katika kipindi 
cha miaka mitano hadi saba Maria Sharapova, Ana Ivanovic , Maria Kirilenko na Anna Kournikova wamekuwa wakiingia katika headlines ya magazine tofauti tofauti.
1- Eugenie Bouchard ni mchezaji tennis kutokea Canada, mrembo huyu ana umri wa miaka 21 lakini anatajwa kama mmoja kati ya wanamichezo wa kike wanaolipwa fedha nyingi.
2- Sorana Cîrstea ni mrembo kutokea Romania
 ana umri wa miaka 25, mara nyingi huwa haonekani akishika nafasi za juu
 katika mchezo wa tennis ila anatajwa kuwa ni moja kati ya wachezaji 
tennis warembo kutoka bara la Ulaya.
3- Sania Mirza ana umri wa miaka 28, ukitaja moja kati ya warembo kutoka India basi Sania Mirza huwezi kuacha kumuweka katika list hiyo. Uzuri na urembo wake ni wakuvutia.
4- Maria Sharapova
 ni mrembo wa kirusi na anashika namba 2 katika viwango vya mchezo wa 
tennis ana umri wa miaka 28, anatajwa kuwa kati ya wanamichezo 
wanaolipwa nyingi.
5-  Caroline Wozniacki ana umri wa miaka 25 raia wa Denmark, ni moaja kati ya wachezaji tennis maarufu sana na amewahi kuiwakilisha nchi yake katika mashindano mbalimbali ikiwemo US Open na Australian Open.
6- Ana Ivanovic ni mrembo kutokea Serbia
 yupo katika hii list ya wachezaji tennis warembo, ana umri wa miaka 27.
 Amewahi kutokea mara kadhaa katika magazine za michezo ila mwaka 2013 
alikuwa katika list ya wasichana 100 warembo.
7- Agnieszka RadwaÅ„ska
 aliwahi kushika namba 2 mwaka 2012 katika viwango vya mchezo wa tennis,
 ameshiriki na kufika katika hatua ya nusu fainali katika michuano 
tofauti tofauti. ana umri wa miaka 26 anatokea Poland.
8- Victoria Azarenka ni mrembo mwenye umri wa miaka 26 anatokea Belarus nae yupo katika hii list ya wachezaji tennis warembo, amewahi kushinda taji la Australian Open lakini alikuwa namba moja katika viwango vya wachezaji tennis kwa mwaka 2012.
9- Simona Halep kutokea Romania
 ana umri wa miaka 23 ni moja kati ya wachezaji tennis mahiri, mwaka 
2014 alikuwa namba 10 ya katika viwango vya ubora wa wachezaji tennis.
10- Garbiñe Muguruza ni moja kati ya wachezaji tennis wanaochipukia Hispania, amefanikiwa kuingia katika top 10 ya viwango vya wachezaji tennis wa kike, umri wake ni miaka 21


No comments