Maneno ya Nicki Minaj kuhusu Drake & Meek Mill + beef yake na Miley Cyrus!
First lady wa label ya Cash Money Records Nicki Minaj ameingia kwenye headlines za burudani baada ya interview yake na jarida la The New York Times Magazine, miongoni mwa majarida makubwa ya mastaa wa kike wa HipHop Marekani.
Akiwa kwenye interview na jarida hilo Nicki Minaj alizungumzia vitu vingi baadhi vikiwa mtazamo wake kuhusu beef ya Drake na mpenzi wake Meek Mill pamoja na beef yake na Miley Cyrus msanii wa Pop nchini Marekani... kwenye mazugumzo Nicki alikuwa na haya yakusema kuhusu Miley Cyrus..
>>> ”
kitendo cha yeye kukasirishwa na nilichokisema kuhusu kitu
kinachowagusa wanawake weusi kinanifanya nimchukulie tofauti. Yeye kila
siku yupo kwenye videos na watu weusi haswa wanaume na mara nyingi
anawaaakila wasanii wa weusi wa kike kwenye majukwa yake tofauti, lakini
eti hutaki kujua wanawake weusi wanajisikia vipi kuhusu vitu muhimu
vinavywagusa (kama ile tuzo)!? Sio kweli, huwezi kutaka mazuri tu kuhusu
sisi bila kupenda au kuelewa mabaya yanayotuzunguka. kama anapenda
kuenjoy lifestyle yetu na kuwa karibu na sisi, kuimba na kuperform na
sisi basi inabidi ajue yale mambo yanayotugusa na kutuumiza pia, na sio
tofauti!” <<< Nicki Minaj.
Na alipoulizwa kuhusu beef ya Meek Mill na Drake, Nicki Minaj alikuwa na haya ya kusema…
>>> “Wale
ni watu wazima, watu wazima wenye akili zao timamu… hii issue ni kati
yao wawili wao ndio wanajua wanaipeleka wapi hii beef… ila binafsi
siipendi, sijiskii vizuri kuwaona wakiwa hivyo, na siku zote maamuzi ya
busara ni kutokuchagua upande haswa issue ikiwa inawahusu watu wawili
unaowapenda. Kwanza ni ujinga. Nataka tu yaishe soon.” <<< Nicki Minaj.
Badaae Nicki Minaj akaulizwa kuhusu baba yake aliewakimbia na kama amechangia kwa kiasi kikubwa kwa yeye kuwa na ubabe alionao leo, Nicki alijibu hivi…
>>> “Yule
alikuwa katili sana. Kwanza mara nyingi nilikuwa namsikia anagomba na
kutukana sana, mara nyingi! Na hiyo ilinifanya nikue nikijua hiyo ndio
namna ya kuishi, kwa sababu ndivyo nilivyokuwa nikikua na kumuona
anaishi!” <<<Nicki Minaj.
No comments