Sandra Awataka Aunt, Sajent Kunyonyesha


STAA wa filamu Bongo, Salama Salmini `Sandra’ amewataka wasanii wenzake, Aunt Ezekiel na Husna Idd ‘Sajent’ kuwanyonyesha watoto wao na kuachana na imani kuwa kufanya hivyo kutawachakaza.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Sandra alisema wasanii hao muda mwingi wanaonekana kwenye kampeni wakati wana watoto wachanga, hivyo aliwasihi kuhakikisha wanawanyonyesha ili kuwasaidia katika ukuaji bora kwani ana hofu huenda hawapati muda wa kuwanyonyesha.
“Aunt na Sajent muda mwingi nawaona wapo kwenye kampeni, watoto wao bila shaka wanawaacha nyumbani na mahausigeli, ni wazi suala la kunyonyesha hapo halipo, nawashauri wajitahidi kunyonyesha watoto wao sababu  maziwa ya mama ni muhimu sana kwa mtoto, ndiyo maana mimi hunioni kwenye kampeni japo ni CCM na hata ningeenda nisingemuacha mwanangu, maana ndiyo kwanza ana miezi mitatu,” alisema Sandra.
Chanzo:GPL

No comments

Powered by Blogger.