Hizi ndizo sababu za Bonge la Nyau Kudatishwa na Irene Paul


Urembo na uchapakazi wa mwanadada anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu, Irene Paul umemdatisha msanii wa muziki, Bonge La Nyau aka Nyauloso.
Nyauloso ameiambia Nje ya Box ya kipindi cha Planet Bongo cha EATV, kuwa anatadishwa mno na miondoko ya mwanadada huyo.
“Irene Paul kwanza ukiachana na mambo yote mimi ni shabiki yake,” alisema rapper huyo.
“Ni mtu ambaye nakuwa naangalia sana kazi zake. Lakini ni mtu ambaye mimi mwenyewe nikimuona najihisi kuna kitu. Unajua yule ni mzuri, ni mtu ambaye nilikuwa nikikutana naye toka zamani nahisi kuna kitu kwenye mwili wangu. Lakini wala hatujawi kuonana, nahisi pia haya mambo hayafahamu,” alisema Bonge la Nyau.
Pia Nyauloso alieleza sababu za kuendelea kuwa na kigugumizi na kushindwa kujikaza kisabuni kwenda kumweleza mrembo huyo kile moyo wake unataka!
“Vipo vingi vinavyonizuia,” aliendelea Loso. “Kwanza hatuna ukaribu, anaweza akawa ananijua kwa sababu na mimi pia ni msanii wa Bongo Flava, lakini hatuna ukaribu. Na kitu kingine siwezi jua yupo katika relation na nani? Unaweza ukaenda kumwambia mtu kwa sababu hizi ni hisia zako halafu asizifanyie kazi. Bora niendelee kuwa na duku duku. Irene Paul mimi namwambia kwanza ana mashabiki wengi kwahiyo aongeze juhudi kwenye kazi zake.”
Chanzo:Bongo 5

No comments

Powered by Blogger.