Mastaa wa kimarekani wampongeza DIAMOND baada ya kushinda tuzo ya mtv ema 2015…..

Mwaka huu umekuwa mzuri sana kwa mtu wetu Diamond Platnumz baada ya kushinda tuzo nyingi ya kimataifa  MTV EMA 2015 jijini Milan Italy.

Ushindi wa tuzo ya MTV  kwa Diamond Plantumz si ushindi mdogo bali ni heshima kwa Tanzania kwani hata staa wa marekani naye amemiliki headlines za kumpongeza kwa ushindi wa tuzo hiyo.

Staa huyo baada ya kuziona picha na video za jinsi  Diamond Platnumz  alivyotwaa tuzo hiy  ilibidi aandike haya maneno.’.CONGRATS TO MY HOMIE@diamondplatnumz for winning#BestWorldWideAct at the#MTVEMAs Keep being great, Let’s go get em’ my guy..’aliandika Neyo katika ukurasa wake wa instagram.

Pongezi hizo hazikuishia kwa Neyo kwani baada ya saa chache zilizopita naye rapper na producer wa muziki kutoka Marekani Swizz Beatz akampongeza Diamond Platnumz kwa ushindi huo.

No comments

Powered by Blogger.