‘Cinderella’ ya Alikiba iliuza Mil. 200, matumizi je? swali la ‘Kidoti’? Haupendi wimbo wake? Majibu haya..
Kwenye show ya XXL alhamisi ya November 12 2015 mgeni aliyealikwa alikuwa ni Alikiba ambaye alikuja kuzindua mdundo wa ngoma mpya ambayo wameshirikiana na Christian Bella… lakini kuna story za zamani hivi nazo ziliguswa pia.
Unajua Alikiba akiisikia ngoma ya ‘Usiniseme’ anakumbuka wapi? >>> ‘Nakumbuka safari zangu kwenda G Records, ilikuwa ni lazima niende nikashinde na Producer wangu KGT kila siku hata kama sina kazi‘
Ana mpango wa kuachia album? >>> ‘Nitatoa
album mwakani kwa mfumo wa digital nikimpata msambazaji mzuri… nataka
kufanya album kali sio nijaze tu nyimbo kwenye album… nakumbuka album ya
kwanza niliyonunua ilikuwa album ya AY, halafu nikanunua ya Matonya… ni kuonesha tu kwamba najali muziki…’
Alikiba aliachia album ya Cinderella mwaka 2009, anajiona wapi toka mwaka huo >>> ‘Najiona kama kiwango changu kimekua sana… sipendi wimbo wa ‘Shababi’ kwa sababu najiona niliimba chini ya kiwango‘
Mauzo ya Cinderella je? Matumizi yake? >>> ‘Cinderella
ilivunja rekodi na sijawahi kusikia kama kuna album nyingine iliwahi
kuizidi mauzo… iliuza nakala milioni mbili, kila copy nilikuwa nachukua
shilingi 200… jumla inakuwa kama Mil. 200 hivi sema wakati ule utoto
mwingi ila nilifanikiwa kujenga.’
Presenter wa XXL, Adam Mchomvu akachomekea swali kuhusu Kidoti, majibu yaliyotoka ni haya hapa >>> ‘Mjasiriamali, bishosti kanyooka, yuko fresh… yap… full stop‘- Alikiba.
No comments