Sentensi mbili za David Beckham kama Cristiano Ronaldo ataondoka Real Madrid …
Kama ni mpenzi wa soka wa muda mrefu huwezi kuacha kumjua David Beckham staa wa zamani wa soka wa Man United, Real Madrid na timu ya taifa ya Uingereza, Beckham ni mchezaji ambaye jezi yake namba saba ilirithiwa na Cristiano Ronaldo wakati ambao Beckham alitimkia Real Madrid ya Hispania huku Ronaldo akijiunga na Man United.
Beckham
 ambaye alikuwa akisifika kwa umahiri wake wa kupiga mipira ya faulo 
kauli yake imeingia katika headlines baada ya kufunguka katika interview
 kuwa kama Cristiano Ronaldo atahama Real Madrid ni vizuri akirudi Man United, kauli ambayo inazidi kuongeza uvumi wa staa huyo kuhama Real Madrid ya Hispania.
“Sikuwahi
 kumshauri yoyote kurudi Man United, Cristiano amekuwa kama shabiki wa 
Man United kwani anaipenda na amefanya vizuri akiwa  Old Trafford na 
kucheza kwa bidii” >>> Beckham
“Kila 
mmoja ambaye amewahi kucheza na Ronaldo angeongea haya, Ronaldo sio tu 
ni moja kati ya wachezaji waliokuwa na vipaji vikubwa katika soka bali 
ni mchezaji anayejituma, binafsi kama ataondoka Real Madrid sehemu 
sahihi nafikiri anayoweza kwenda ni Man United” >>> Beckham
Hadi sasa Cristiano Ronaldo ambaye anachezea timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid amekuwa akihusishwa kuhama Real Madrid na kwenda katika klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, kurudi Man United ya Uingereza au kwenda kucheza soka Marekani
 mahali ambapo aliripotiwa kununua jumba la kifahari kwa miezi ya hivi 
karibuni kitu ambacho kinahusishwa na maandalizi ya staa huyo kuhamia Marekani.


No comments