Hatma ya Jose Mourinho Chelsea imeingia katika headlines ya magazeti ya Uingereza October 26

Bado mashabiki na wapenzi wa soka duniani kote wanajadili juu ya mwenendo wa klabu ya Chelsea kama Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu UingerezaChelseaambayo inafundishwa na Jose Mourinhokwa awamu ya pili sasa imekuwa haipati matokeo mazuri kwa siku za hivi karibuni na kwa sasa ipo nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi huku ikiwa na point 11.

Kufuatia mwenendo mbovu wa timu hiyo stori kutoka katika magazeti yaUingereza ya leo October 26 yanaeleza kuwa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich huenda akamfuta kazi Jose Mourinho kwa mara ya pili kama timu yaChelsea ambayo itacheza mechi naLiverpool katika uwanja wake wa nyumbani Jumamosi ya October 31 itafungwa.

Taarifa kutoka katika vyombo vingi vya habari Uingereza zinasema kamaChelsea atafungwa na Liverpool Stamford Bridge basi mmiliki wa klabu yaChelsea Roman Abramovich atamfuta kazi Jose Mourinho, kama Mourinhoakifukuzwa Chelsea itakuwa ni mara ya pili kufukuzwa kazi baada ya kufukuzwa kwa mara ya kwanza 2007 na kurejea 2013. Nafasi ya Mourinho Chelseainatajwa kuchukuliwa na Carlo Ancelottiau Guus Hiddink

No comments

Powered by Blogger.