Haya ndio maneno ya Rihanna kuhusu Chris Brown sasa hivi…
Siku chache zilizopita Rihanna alifanya interview
na gazeti la Vanity Fair, la Marekani na
kuzungumza vitu vingi ikiwemo mahusiano yake
ya zamani na R&B superstaa Chris Brown.
Rihanna kwenye cover la Vanity Fair Magazine
mwezi huu.
Baada ya kujibu maswali mengine yote, maswali
juu ya yeye na aliewahi kuwa mpenzi wake
Chris Brown yalifuata… kwenye kuzungumza
Rihanna alisema kuwa licha ya yote yaliokuwa
yanatokea kati yake na Chris Brown staa huyo
bado alikuwa anajaribu kulinda hisia alizokuwa
nazo juu yake lakini sasa hivi hana uhusiano wa
aina wowote ule na Chris Brown ila bado
anamjali sana staa huyo…
Rihanna: (VF Photo Shoot)
>>> “Nilikuwa najaribu sana kumlinda Chris, yeye
pamoja na hisia zangu juu yake… mara nyingi
nilikuwa nahisi watu hawamuelewi, hata baada ya
ile issue kutokea na watu kuongea… lakini unajua
inakuwa ngumu ya wewe kuona picha halisi ya
mtu na jinsi mambo yalivyo kama bado
umekumbatia baadhi ya vitu fulani, haswa ukiwa
bado unahitaji the best kutoka kwa mtu husika, na
ukiwakumbusha makosa yao, au ukiyakumbuka
yale matukio yaliokuumiza maishani, au hata
ukijaribu kuonyesha kuwa upo tayari kuvumilia
kitu au mtu, wataishia kukufikiria vibaya na
kukushusha hadhi.. . “ <<< Rihanna.
Rihanna: (VF Photo Shoot).
>>> “… na ukijaribu kuvumilia, labda kwasababu
unajaribu kujiridhisha kuwa pengine hiki ndicho
[unachokistahili na kukihitaji] sasa hapo ndipo
unapoanza kugundua kuwa ‘mmmh’ nilikuwa
mjinga kuamini kitu hiki kinanifaa. Sometimes
maamuzi sahihi na salama ni kuachana na hicho
kitu… simchukii, namjali sana na nitaendelea
kumjali mpaka siku nitakayokufa… ila tu mimi na
Chris sio marafiki na sio kwamba mimi na yeye ni
maadui pia. Imetokea tu hatuna uhusiano wowote
sasahivi.” <<< Rihanna.
No comments