EXCLUSIVE: SAMATTA ATOA KAULI NZITO KABLA YA KUIKABILI MALAWI
Mshambuliaji wa kimataifa wa
Tanzania anaecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya TP Mazembe ya nchini
Congo DR amesema hatoshangaa endapo mashabiki wa soka nchini watawalaumu
wachezaji wa Stars kwa kushindwa kuifunga Malawi kwenye mchezo wa leo.
Samata amesema Stars inabidi
ishinde mchezo wake wa leo dhidi ya Malawi kwasababu viwango vya timu
zote mbili vinalingana kwa kiasi kikubwa. Licha ya kusema Stars ni
lazima ishinde mbele ya Malawi, lakini amesisitiza kuwa inabidi ishinde
kwa idadi kubwa ya magoli huku yeye akikataa kuahidi chochote kwenye
mchezo huo.
“Siwezi kuahidi chochote
kwasababu ahadi ni deni na usipolitimiza ni dhambi, ila nadhani kwamba
tunaenda kupambana na siichukulii Malawi kama Nigeria, nafikiri Malawi
ni timu ya kiwango chetu na nita-appreciate watanzania kama watatulaumu
kwanini hatujaifunga Malawi”, amesema Samatta ambaye tayari ameshafunga
magoli sita baada ya kucheza mechi nane kwenye ligi ya vilabu bingwa
barani Afrika.
“Lazima tuifunge Malawi hakuna
matokeo mengine ambayo tunayataka na ni lazima tumfunge kwa idadi kubwa
ya magoli, yani lazima iwe hivyo”, amesisitiza Samatta ambaye anatarajia
kucheza fainali ya ligi ya mabingwa Afrika siku chache zijazo akiwa na
TP Mazembe.
No comments