Aunty Lulu Anaswa kwa Sangoma
MSANII wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amenaswa kwa sangoma mkoani Tanga ‘akitengenezwa’ ili kung’arisha nyota yake inayodaiwa kushuka.
Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili kuwa kimemshuhudia msanii huyo akiwa kwa sangoma maeneo ya Handeni alikokaa kwa muda wa wiki moja sasa.
“Mh, mmejuaje hayo? Kweli nipo Tanga kwa ndugu wa baba yangu, nimekuja kufanyiwa tambiko maana mambo hayaendi vizuri likiwemo suala la mapenzi, naachwa kila siku wanaolewa wengine, ndo maana nimeamua kuja huku kabisa maana nimechoka kwa kweli ila nitarudi Dar siku mbili hizi,” alisema msanii huyo
Chanzo: GPL
No comments