Dr Cheni Afungukia Tatizo ya Umeme Kuyumbisha Soko la Filamu


Msanii wa filamu, Dr Cheni amesema kuwa biashara ya filamu kwa sasa imeshuka kutokana na tatizo la umeme linaloendelea.
Dr Cheni ameambia Bongo5 kuwa mawakala wanalalamika kushindwa kuuza kazi za filamu kama walivyotarajia kutokana na tatizo la umeme.
“Soko la filamu sasa hivi linasumbua kutokana na haya matatizo ya umeme,” amesema Cheni. “Umeme ukisumbua na soko la filamu linayumba kwa sababu sisi wateja wetu wanatumia umeme, sasa hata wazalishaji wa kazi zetu wanaogopa kuzalisha kazi nyingi kutokana na kutonunulika sokoni. Yaani kwa kifupi soko limesimama. Wewe nenda kwa mawakala pale Kariakoo watakwambia. Kwahiyo ukiona tatizo la umeme ujue na sasa kazi zetu zinasimama.”
Chanzo: GPL

No comments

Powered by Blogger.