Jayjay Nimeumizwa na Mapenzi!


MAUMIVU niache! Msanii wa filamu ya Who Is My Child, Janeth Jackson ‘Jayjay’ amekiri kuumizwa na kulizwa na mapenzi mara kwa mara licha ya kuwa na muonekano wenye mvuto machoni kwa wanaume jambo linalomnyima amani ya maisha.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Jayjay alisema si rahisi kwa watu kuamini ukweli huo kutokana na uzuri wake wa umbo na sura, lakini ukweli ni kwamba hana furaha juu ya mapenzi kufuatia wanaume wengi kumtumia kisha kumkimbia bila kutimiza ahadi zao.
“Sina furaha na mapenzi, nimeumizwa sana na wanaume kila anayekufuata anakuahidi mambo mengi lakini akishatimiza haja zake anakimbia, kwa sasa sitaki tena mapenzi,” alisema Jayjay na kuongeza kuwa sasa anataka kujikita zaidi katika kazi.
Chanzo:GPL

No comments

Powered by Blogger.