Ana miaka 9 tu! afanya maajabu kwenye mti huu huko Kenya.





Kenya imekuwa ikiingia kwenye headline mara nyingi kutokana na kuwepo na matukio mbalimbali ambapo safari hii wakazi wa Kararia Marakwet bado wanajiuliza uwezekano wa Mvulana mwenye umri wa miaka 9, kuweza kuurudisha mti katika hali yake ya kuoteshwa ambao ulikuwa umeanguka chini na ulikuwa ukikatwa kuni miaka mitatu iliyopita kwa kuunyanyua peke yake bila kusaidiwa na mtu yoyote .

Richard Komen mzazi wa mwanafunzi huyo amesema mtoto wake amekuwa na tabia za kufanya matukio ya  kushangaza tangu kuzaliwa kwake.
Nimekuwa nikijaribu kuelewa alivyofanya, nilipomuuliza alisema aliunyanyua mara ya kwanza kisha akapumzika kidogo na kisha akauinua tena mara ya pili hapo ndipo mti huo ulirejelea uhai wake” alisema Komen.
Watoto waliokuwa eneo hilo wamesema mvulana huyo aliwaambia wasogee pembeni kwa sababu alitaka kurejesha mti huo kama ulivyokuwa umeoteshwa awali, huku Kina mama wa eneo hilo wakisema mti huo uliangushwa na upepo mkali msimu wa mvua mwaka 2011, na wamekuwa wakiutumia kwa kukata kuni kwa matumizi ya nyumbani.

No comments

Powered by Blogger.