Salama Jabir: Nitarudi kwenye redio, panapo majaaliwa
Licha ya kuwa mtangazaji bora wa TV wa kipindi cha Mkasi kilichoshinda tuzo mbili kwenye Tuzo za Watu, Salama Jabir aliwika mno kwenye redio.
Alikuwa na kipindi maarufu, Planet Bongo kupitia East Africa Radio lakini aliamua kujikita zaidi kwenye TV. Akiwa na kipindi kipya kwa sasa, Ngaz Kwa Ngaz kinachoruka kila Alhamis, EATV, Salama amedai kuwa panapo majaaliwa siku za usoni anaweza kurejea tena redioni.
Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, Salama alisema amekuwa na mambo mengi mno anayofanya kwa sasa na kwamba hapendi kuongeza vingine kiasi cha kumfanya asivifanye kwa uweledi.
“Hiyo plan ipo ya kufanya redio so hopefully mambo yakikaa sawa tukijaaliwa uhai na uzima then tutarudi kwenye redio,” alisema.
Hata hivyo alikiri kuwa kwa sasa si msikilizaji mzuri wa redio za Bongo. Alidai kuwa vituo vingi vya redio vimekuwa na vipindi kama fashion show na vingi vinaigana sana.
“Mimi sio mtu wa kusikiliza redio sana kwasababu rdio sasa hivi imekuwa kama fashion show,” alisema Salama kwenye kipindi hicho.
Hata hivyo hakusita kumsifia mtangazaji wa The Playlist, Lil Ommy kuwa amekuwa na kipindi cha tofauti na anakipenda.

No comments