Birdman ajipendekeza kwa Lil Wayne, ampongeza katika siku yake ya kuzaliwa

Rapper Birdman ameweka tofauti zake (kwa muda) na Lil Wayne na kuamua kumtakia heri ya kuzaliwa msanii huyo waliyepelekana mahakamani.
14504848_1102323033196713_8123643685029019648_n
Kupitia mtandao wa Instagram, Birdman amepost picha nne ambazo aliwahi kupiga na Lil Wayne na kuandika, “HBD MY SON @liltunechi#BEFORE ANYTHANG #CMR uptownshit#BMJR #ymcmb4life #bloodlove.”
Wawili hao waliingia kwenye ugomvi mzito tangu mwaka jana huku rapper huyo akitaka lebo yake ya Cash Money kumlipa kiasi cha dola milioni 51 kwa kuchelewesha kuachia albamu yake iliyotakiwa kutoka mwaka 2014.

No comments

Powered by Blogger.