Zlatan Ibrahimivic ajibu muda atakaokaa United
Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic (34) amedai kuwa anaweza akaongeza mkataba wake wa kukaa zaidi kwenye timu hiyo.Mchezaji huyo alisajiliwa kwenye dirisha la usajili msimu huu na United kwa mkataba wa mwaka mmoja kama mchezaji huru akitokea PSG. Akiongea na Sky Sports, Ibrahimovic ameongeza kuwa hata wachezaji wengine wa nje ya timu hiyo wanatamani kuichezea timu hiyo.
“Let’s see what happens. You never know. It could be more than two, it could be more than three. Let’s see how long I feel like I can perform. I will not be somewhere only because I am Ibrahimovic. I will be somewhere because I can perform and bring results,” alisema.
“It was the moment to come to England, and who would not come to Manchester United? I don’t believe there is anybody who could say no to a club like Manchester United. Probably the players that play for other clubs in England would like to come here, 100 per cent. I am very happy I am here and representing Manchester United. Even the name sounds cool,” aliongeza.
Ibrahimovic alikuwa ni mchezaji wa pili kati ya wachezaji wanne waliosajiliwa na United kwa msimu huu chini ya kocha wao mpya Jose Mourinho na anatarajiwa kuanza kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya AFC Bournemouth siku ya Jumapili.
No comments