Tyga matatani,jaji aamrisha akamatwe kwa kukacha mahakamani
Kwa mujibu wa TMZ, Rapper huyo alishindwa kutokea mahakamani Jumanne hii ambako alikuwa anatarajiwa kujitetea kwenye kesi ya kudaiwa kodi ya nyumba ya $480,000 anayodaiwa na mwenye nyumba aliyokuwa amepanga.
Kutokana na kutoonekana, jaji ameamuru rapper huyo akamatwe na hivyo kukaa jela.
Pamoja na kushindwa kulipa fedha hizo, Tyga amekuwa akiishi maisha ya kifahari ikiwemo hivi karibuni kumnunulia mpenzi wake Kylie Jenner gari aina ya Maybach yenye thamani ya $200,000 kwenye birthday yake
Mwenye nyumba huyo alimtimua Tyga kwenye mjengo wa Malibu na kumwacha akitangatanga.
Alihamia kwenye nyumba Bel-Air, anakodaiwa kulipa $46,000 kwa mwezi.
No comments