Drake afunguka kumtamani Rihanna

drake-rihanna-ovo-fest
Penzi ni kidonda ukiwaza utakonda. Rapper wa Canada, Drake ameonyesha kutamani kuwa na mahusiano na Rihanna.
Rapper huyo aliyekuwa akifanya show wikiendi hii kwenye ukumbi wa Madison Square Garden, New York amesema kuwa anapata upendo wa dhati kutoka kwa Rihanna na anatamani sana kama angekuwa na mahusiano nae kwani yeye pia anamkubali sana mrembo huyo.

“If you`ve got love for Rihanna in New York City, Cuz you know i`ve got love for Rihanna,” alisema Drake kwenye tamasha hilo.

Hivi karibuni zilienea tetesi za wawili hao kurudiana na kuonekana pamoja sehemu mbalimbali lakini baadaye tetesi hizo zilipotea baada ya Drake kuhusishwa kuwa na mahusiano na mwanamitindo, Hailey Baldwin (19).

No comments

Powered by Blogger.