Mzee Chilo Awashukia Wasanii Kuhusu Kunyonywa na Wadosi
Msanii mkongwe wa filamu nchini, Mzee Chilo amesema siyo kweli kwamba wasambazaji Wakiindi wanawanyonya wasanii wa filamu.Jumapili hii, Mzee Chilo amesema kuwa wasanii wengi kwa sasa wanafanya filamu mbovu ndio maana filamu zao zinakosa soko kwa Waindi.
“Wanaosema kwamba bongo movie imeshuka sijui hizi taarifa wanazipata wapi, mimi nipo kwa miaka mingi na wasambazaji wakiindi na sijawai kupata tatizo lolote kusema kweli,” alisema Chilo. “Mimi nadhani wanaosema Waindi wanaaribu soko la filamu siyo kweli, huo ni uongo, wao ndio wanafanya filamu mbovu ndio maana hazifanyi vizuri,”
Muigizaji huyo amewataka wasanii wa filamu kufanya kazi kwa bidii na kuacha kulalamika.
No comments