Staa wa soka Uingereza ahukumiwa miaka 6 jela kwa kujihusisha kimapenzi na mtoto
March 24 2016 headlines za habari za 
kusikitisha katika ulimwengu wa soka zimezidi kutawala, ikiwa umepita 
muda mchache tu toka utangazwe msiba wa nguli wa soka wa Uholanzi na FC 
Barcelona Johan Cruff, ila zimetoka taarifa za staa wa soka kufungwa 
jela.
March 24 winga wa zamani wa klabu ya 
Manchester City na timu ya taifa ya Uingereza Adam Johnson amehukumiwa 
miaka sita kwenda jela baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha 
kimapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15.
Adam Johnson akitoka mahakamani
Adam Johnson hadi anahukumiwa kifungo 
hicho alikuwa anaitumikia klabu ya Sunderland ya Uingereza, ambayo toka 
mwaka 2012 alijiunga nayo hadi 2016, ameichezea jumla ya mechi 122 na 
kuifungia magoli 19.


No comments