NEY WA MITEGO Amemdiss Gigy Money?, Haya Ndio Aliyoyasema

Nay wa Mitego amemdiss Gigy Money?Asema hana Sura nzuri lakini amejaliwa.
Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa video Queen anayetamba kwa sasa Gigy Money kwenda kwa rapper wa Shika adabu yako Nay wa Mitego kuhusiana na uhusika wake kwenye video ya wimbo huo.
Gigy ameweka wazi kuwa alipewa Shilingi elfu ishirini tu kutoka kwa rapper huyo kama malipo ya kutokea kwenye video hiyo na pia amelalamika kuwa walikubaliana yeye aonekane kwenye kipande kinachohusu wanachuo lakini baadala yake ameoneshwa kwenye kipande kinachohusu mwanamke mwenye sura mbaya.
Alipoulizwa Nay wa Mitego,kwa upande wake yeye hakumwita Gigy wala hawakukubaliana chochote kwani director ndiye alimwita na yeye alimpa elfu 20 kama nauli tu ya bajaj.
Kuhusiana na uhusika wake,Nay amesema kuwa yeye hakuwepo wakati wanashut lakini alipomwona Gigy alihisi kipande kinamchomfaa ni kile cha mwanamke mwenye sura mbaya kwani Gigy hana Sura nzuri.
“Gigy hana sura nzuri,bhasi vile amejaliwa kibonge kibonge,yeye kukaa kwenye kipande kile nime suggest mimi..Sio uongo ukiwaita wanawake warembo Gigy yupo?ila ndio hivyo amejichetua watu wamemfahamu bhasi“alifunguka Nay.

No comments

Powered by Blogger.