TETESI: MOURINHO AKARIBIA KUWA MENEJA WA MANCHESTER UNITED

Kuna taarifa zilizozagaa leo katika vyombo vya habari barani Ulaya kuwa kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho anakaribia kukubali na kusaini mkataba wa kuwa meneja wa Manchester United kwa msimu wa 2016/2017.

Mtandao wa habari wa Sky Sport Italia umethibitisha kuwepo kwa taarifa hizo. Mreno huyo anayesemwa kuwa moja kati ya makocha bora na wenye mafanikio makubwa barani Ulaya amekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na ‘mashetani wekundu’ Manchester United tangu atimuliwe kibaruani na klabu ya Chelsea.

Taarifa zinaeleza zaidi kuwa Mourinho ameamua uamuzi huo wa kujiunga na Manchester United siku chache baada ya klabu ya Manchester United kutangaza ujio wa kocha wa Bayern Munich Mhisipaniola Pep Guardiola.

Mourinho ambaye alikuwa na uhasimu mkubwa sana na Guardiola walipokuwa wote katika ligi kuu ya Hispania La Liga kama atafanikiwa kujiunga na Manchester United basi watafanikiwa kurejesha uhasimu wao kwa mara nyingine tena.

Kwa sasa klabu ya Manchester United ipo katika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu England ikiwa na pointi 40 nyuma ya Arsenal iliyopo nafasi ya 4 kwa jumla ya pointi 45.

No comments

Powered by Blogger.