Sports ::MESSI AWEKA REKODI NYINGINE KWENYE MAISHA YAKE YA SOKA

Leo Messi ameandika rekodi nyingine tena kwenye maisha yake ya soka wakati FC Barcelona ikiiangushia kipondo ‘heavy’ timu ya Valencia kwenye mchezo wa kombe la mfamle Hispania maarufu kama Copa del Rey.
Magoli mawili ya mapema kutoka kwa Luis Suarez yaliwapanguvu watoto wa Catalan kabla ya Leo Messi kutandika bao na kuipa timu yake uongozi wa bao 3-0 kabla ya kwenda mapumziko.
Kipindi cha pili baada ya Neymar kukosa penati, Messi aliingia tena wavuni kuiandikia timu yake bao la nne. Goli hilo lilikuwa special kwake kwasababu lilikuwa ni bao lake la 500 kwenye maisha yake ya soka.
Goli hilo lilimfanya Messi afikishe magoli 435 akiwa Barcelona, amefunga magoli 49 akiwa na timu ya taifa ya Argentina, magoli 14 akiitumikia Argentina U20, na magoli 2 akiwa na Argentina ya U23.

No comments

Powered by Blogger.