Hizi ni taarifa mbaya kwa Chelsea kuhusu mpango wa kumsajili staa huyu …
Klabu ya soka ya Chelsea
ambayo ilikuwa na matumaini kwa kiasi kikubwa kupata saini ya moja kati
ya wachezaji wa kibrazil, January 19 imekataliwa kuuziwa mchezaji na
klabu inayo mmiliki. Chelsea ambayo kwa sasa ipo na kocha wa muda Guus Hiddink ilikuwa inahitaji kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea klabu ya Shakhtar Donetsk Alex Teixeira.
Chelsea walikuwa wanatajwa kwa karibu kuwa katika mipango ya kuishawishi klabu ya Shakhtar Donetsk iwauzie Alex, ila uongozi wa klabu hiyo January 19 unaripotiwa kutoa taarifa za kutokuwa na mpango wa kumuuza Alex hususani katika dirisha hili dogo la usajili la mwezi January.
Staa huyo ambaye kama angejiunga Chelsea angekutana na wabrazil wenzake kama Ramires na Oscer, anatajwa kuivutia Chelsea hususani kwa wastani wake wa sasa kucheza mechi 15 akiwa na klabu ya Shakhtar Donetsk na kufunga magoli 22
No comments