Usain Bolt kwenye headlines moja na Steven wa Yanga ? mrembo huyu kasabisha (+Pichaz)
Mwanariadha wa kijamaika ambaye amewahi kutajwa kama moja kati ya viumbe vyenye kasi zaidi duniani Usain Bolt ameingia kwenye headlines kisa mrembo Patty Lopez de la Cerda, mwanariadha huyo aliwahi kuweka rekodi ya Dunia kwa kukimbia mbio za mita 100 kwa muda mchache zaidi.
Unafahamu michezo ya kubet yaani
kutabiri matokeo ya kwa njia ya teknolojia ya kikompyuta ambayo kwa sasa
imekuwa maarufu sana ndani ya jiji la Dar Es Salaam, stori ya nyota wa riadha Usain Bolt ameponzwa na mchezo wa kubet, Bolt ambaye ni shabiki wa klabu ya Manchester United ilimlazimu kuvaa jezi ya Arsenal bila kupenda.
Bolt alikubaliana na mtangazaji wa kike wa kimexico Patty Lopez de la Cerda kuwa kama Arsenal ataifunga Man United timu ambayo anashabikia atavaa jezi ya Arsenal. Bolt alivaa jezi ya Arsenal na kuchukua sehemu ndogo ya video na Patty Lopez de la Cerda na kuweka katika account yake ya Instagram kama sehemu ya kukamilisha ahadi yao ya kufungwa na Arsenal goli 3-0. Huenda ukahisi kaamua kuhama timu kama Steven wa Yanga ila yeye kalipa deni.
Usain Bolt alipiga picha akiwa kavaa jezi ya Arsenal ya nyumbani, mgongoni ikiwa na namba 9.58 ikiwa ni sekunde alizotumia kukimbia katika mbio za mita 100 na kuweka rekodi ya Dunia. Bolt anatajwa kustaafu mbio za riadha mwaka 2017 baada ya kumalizika kwa mashindano ya mbio za Dunia za mchezo huo.
No comments