Ulishawahi kuona mlo wa mchana wa Cristiano Ronaldo? basi nimekuwekea hapa jembe langu
Michuano ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Euro 2016 bado inaendelea kwa michezo kadhaa kupigwa, kwa upande wa timu ya taifa ya Ureno ambao walishinda kwa goli 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Denmark . Baada ya ushindi huo Ijumaa ya October 9 Cristiano Ronaldo alipiga picha za mlo wake wa mchana.
Cristiano Ronaldo
alipost picha ya msosi wake wa mchana aliyokula wakati ambao alikuwa
anajiandaa kurudi kwao ni diet ambayo imekamilika kwa kiwango kikubwa,
kwani kulikuwa na mayai, viazi, nyama, matunda, maji ya kunywa juisi.
Baada ya kuweka picha hiyo katika account yake ya instagram mtandao wa dailymail.co.uk ulichambua kila aina ya chakula kilichomo katika diet hiyo.
Katika ratiba ya chakula cha mchana cha Ronaldo
hakuna chakula ambacho kina asili ya sukari nyingi lengo linatajwa kuwa
ni kulinda mwili wake ili kuendelea kuwa sawa kwa michuano mingine. Ureno walicheza mechi dhidi ya Denmark na kuibuka na ushindi wa goli 1-0, huu ukiwa ushindi wao wa sita katika mechi zao saba za kuwania kufuzu michuano ya Euro 2016.
No comments