Soma hapa mtihani aliopewa falcao na chelsea

Hali si shwari kwa mshambuliaji raia wa Colombia, Radamel Falcao ambaye anaichezea Chelsea kwa mkopo akitokea Monaco, mara baada ya kuambiwa na Mourinho kuwa anahitaji kuonesha uwezo zaidi ya Diego Costa ili aweze kucheza.
Taarifa hizo za kumhusu Falcao, zimevuma wiki hii barani Ulaya huku kukiwa na taarifa ya kwamba huenda akaondoka kikosini hapo January mwakani.
Kuelekea katika mchezo dhidi ya Dynamo Kiev katika michuano ya Ulaya, Falcao pia anatarajiwa kuukosa mchezo huo kutokana na Mourinho kusema kuwa Falcao anahitaji kuonesha kitu zaidi ili acheze kwakua timu yake imekua ikitumia mshambuliaji mmoja.
Maisha yanaonekana kuwa magumu kwa Falcao ambaye alishindwa pia kuonesha makucha yake akiwa na kikosi cha Manchester United msimu uliopita na kuambulia kufunga magoli 4 pekee.
Diego Costa ndiye chaguo namba moja la Mourinho katika safu ya ushambuliaji na hivo kumuweka katika wakati mgumu Falcao mwenye miaka 29.

No comments

Powered by Blogger.