HUU NDIO MSIMAMO WA CHELSEA JUU YA MENEJA JOSE MOURINHO BAADA YA MATOKEO MABOVU

Mmiliki wa klabu ya Chelsea ya Uingereza raia wa Urusi Roman Abramovich tumezoea kuona akifukuza makocha kwa haraka zaidi endapo tu mwenendo wa timu yake utakuwa sio mzuri kwa kipindi kifupi, tabia ya tajiri huyo wa Kirusi imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa kutimuliwa kazi kwa Jose Mourinho kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya.
Wakati wengi wakiwa wanahisi kuwa huenda Jose Mourinho atafukuzwa kazi muda wowote kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa Southampton, mchana wa October 5 tovuti ya Chelsea iliandika ujumbe ambao unatajwa kuwa utaongeza kujiamini kwa timu na kocha, kwani katika kipindi kigumu kama hiki, huwa ni kawaida kwa kocha na wachezaji kupoteza hali ya kujiamini.
“Klabu inaweka wazi kuwa Jose Mourinho ataendelea kuungwa mkono na klabu kama kawaida, licha ya kuwa Jose Mourinho alisema timu imekuwa haina matokeo mazuri na inahitaji kuimarika, hivyo tunaamini tuna kocha mzuri msimu huu na anaweza kuleta mafanikio”>>> 

Chelsea ina wakati mgumu katika msimu huu kwani imecheza mechi nane, imeshinda mbili, sare mbili na kufungwa michezo minne, kwa sasa Chelsea ipo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza. Jose Mourinho aliwahi kuwa kocha wa Chelsea katika kipindi cha mwaka 2004 hadi 2007 na kufukuzwa kazi na mmiliki wa klabu hiyo  Roman Abramovichkabla ya kurejea kwa mara ya pili mwaka 2013.

No comments

Powered by Blogger.