Hivi ndivyo Rihanna alivyoshuhudia Zlatan Ibrahimovic akiweka rekodi hii…
Siku moja baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 34, mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden na klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimović ameweka rekodi nyingine katika soka baada ya kuvunja rekodi ya ufungaji ya muda wote ya Pedro Pauleta ambaye alikuwa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo.
Ibrahimović aliweka rekodi hiyo baada ya kufunga goli mbili katika mechi waliyoibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya wapinzani wao Marseille, Zlatan Ibrahimovic anavunja rekodi ya Pedro Pauleta
ambaye alikuwa anashikilia rekodi hiyo kwa kufunga jumla ya magoli 109
katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2008 wakati akiitumikia klabu hiyo.
Kwa upande wa Zlatan Ibrahimovic aliyejiunga na PSG mwaka 2012 akitokea AC Milan ya Italia amefunga jumla ya goli 110 hivyo Zlatan Ibrahimovic ndio anakuwa mfungaji bora wa klabu hiyo wa muda wote, katika mechi hiyo Zlatan Ibrahimovic alitolewa dakika ya 70 ya mchezo na kupokea tuzo maalum kwa kuweka rekodi hiyo.
Rekodi hiyo iliwekwa mbele ya warembo maarufu duniani ambao ni muimbaji wa Marekani Rihanna pamoja na wanamitindo wa Kimarekani Kendall Jenner na Gigi Hadid, hii sio rekodi ya kwanza kuwekwa na mshambuliaji huyo wa Sweden kwani amewahi kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyeshinda goli katika kila dakika ya mchezo.
No comments