Haya ndiyo matokeo ya match iliyokua ikisubiliwa kwa hamu na mashabiki wengi zaidi duniani.
Manchester united maarufu kama MAN U au RED DEVIL au mashetani wekundu wameshindwa kuonesha uanaume wao dhidi ya clabu ya arsenal maarufu kama the gunners(washika bunduki) na kukubali kipigo cha goli 3 mtungi na kusababisha kushuka kutoka nafasi ya 1 hadi nafasi ya tatu hii leo wakianza manchester city wakifuata arsenal na mashetani hao kushika nafasi ya tatu...
Arsenal wakiwa nyumbani wameonesha uwezo mkubwa kwa kuanza mpira kwa kasi zaidi ambapo man u walionesha kupoyezwa katika kipindi chote cha kwanza,man u walipigwa goli 2 ndani ya dk 7 goli la kwanza likifungwa na sanchez na la pili likifungwa na ozil wakati goli la tatu pia limefungwa kabla ya kipindi cha kwanza kuisha dk ya 19 .
Ikumbukwe kwamba goli zote hizo zimefungwa ndani ya dk 19 tangu mpira kuanza...
No comments