Good News kwa familia ya John Legend na mke wake Chrissy Teigen!!

Familia ya mwanamuziki John Legend na mke wake Chrissy Teigen wanatarajia kufungua ukurasa mpya wa maisha baada ya kutangaza rasmi kuwa ni wazazi watarajiwa.
Baada ya miaka miwili ya ndoa yao huku wakitafuta mtoto hatimaye mkewe ambaye ni mwanamitindo Chrissy Teigen ametangaza rasmi kuwa ni mjamzito.
Katika ukurasa wake wa @Instagram Chrissy amesema wanayofuraha kutangaza kuwa ni mjamzito, na wengi walikua wakifahamu kuwa walikuwa wakijaribu kupata mtoto bila mafanikio, wanashukuru sasa wamefanikiwa.
Wawili hao walianza uhusiano mwaka 2007 na kuamua kufunga ndoa Septemba 2013.


No comments

Powered by Blogger.