Breaking News: Messi kushtakiwa rasmi kwa kosa hili

Shirika la Habari la ufaransa limedondosha habari nzito muda mfupi uliopita: Mwanasoka wa FC Barcelona Lionel Messi sasa atashtakiwa rasmi nchini Hispania.
 Messi atafunguliwa rasmi mashtaka hayo kwa makosa ya kukwepa kodi. Habari hii imekuja kwa mshtuko mkubwa baada ya kuripotiwa mapema wiki hii kwamba uchunguzi ulionyesha hana makosa.
Messi na baba yake wamekuwa wakituhumiwa kukwepa kodi nchini Hispnia kiasi kinachokadiriwa kufikia €4m. Mwendesha mashtaka alisema kwamba Jorge Messi alikwepa kulipa kodi za mapato ya mwanae kwa kutumia makampuni ya nje ya Spain huko Belize na Uruguay kati ya mwaka 2007 na 2009.
Messi na wawakilishi wake siku zote wamekuwa wakikana kuhusika kwa mwanasoka huyo juu ya ukwepaji kodi huko, kwa sababu Leo majukumu yote ya kifedha ameyakabidhi kwa watu wengine.

No comments

Powered by Blogger.