Gigy Money: Nazaa na Idris

gigy-na-idris-2
Msanii wa muziki ambaye pia anafanya ‘modeling’ na utangazaji kwenye Kituo cha Redio cha Choice FM cha jijini Dar, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amejitangazia ushindi wa kumnasa aliyekuwa mpenzi wa Wema Sepetu, Idris Sultan huku akitamba kuwa, sasa atamzalia mtoto.Awali kulikuwa na vita nzito kati ya Wema na Gigy ambapo wakati Wema akiendelea kupalilia penzi lake, Gigy aliibuka na kudai kuwa, atahakikisha anampata Idris akiamini kuwa ndiye mwanaume wa ndoto zake.

Kufuatia vita hiyo ambayo iliibuka baada ya Gigy kunaswa na Idris usiku wakiwa kimahaba kwenye ukumbi mmoja wa burudani uliopo Mikocheni jijini Dar, Wema hakuonesha kujali badala yale aliendeleza msimamo wake kuwa yeye ndiye ‘Mrs’ Idris na wengine waliokuwa wakijipendekeza hawakuwa na chao.

Gigy ajiweka pembeni

Kufuatia Wema kukomalia penzi lake, Gigy alijishtukia na kuamua kukaa pembeni licha ya kwamba mara kadhaa alikuwa akisema kuwa ipo siku atatimiza ndoto yake ya kutoka na Idris.

“Mimi kwa kweli nampenda sana Idris, najua yuko na Wema lakini ipo siku kile ninachokiwaza kitatimia,” alisema Gigy miezi kadhaa iliyopita akionesha kuwa hatakata tamaa kupigania penzi la mshikaji huyo.

No comments

Powered by Blogger.