Dalili nyingine ya Zlatan Ibrahimovic kuelekea kujiunga na Man United
Usiku wa June 9 taarifa za staa wa zamani wa klabu ya Paris Saint Germain ya UfaransaZlatan Ibrahimovichkuhusishwa kujiunga na klabu ya Man United zimechukua sura mpya, Zlatan anaripotiwa kukamilisha hatua ya nne ya kujiunga na klabu yaManchester United.
Dalili inayotajwa kuwa staa huyo yupo mbioni au katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Man United zinazidi kudhihirika, baada ya kuripotiwa tayari ametafutiwa nyumba ya kuishi katika jiji laManchester ambapo ndio makao makuu au mji inapotoka klabu ya Man United.
Kwa mujibu wa nyaraka iliyopostiwa katika websites yaProto Group Ltd ambao ni mawakala wa nyumba inaashiria kuwa mipango yaZlatan kutangazwa kujiunga naMan United ipo tayari kutokana na mji alipotafutiwa nyumba ya kuishi, kwani kabla ya hapo alikuwa akiishi Paris Ufaransa.
No comments