VIDEO: Miaka 13 baada ya Cameroon kumpoteza Foe, JANA tena wamempoteza staa mwingine uwanjani
Ekeng enzi za uhai wake
Ekeng amefariki baada ya kuanguka uwanja dakika ya 70 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Romania uliokuwa unahusisha klabu yake ya Dinamo Bucuresti dhidi ya Viitorul, mchezo ambao ulikuwa unarushwa live kwenye TV, tukio la Ekeng kuanguka limetokea wakati akiwa kasimama peke yake bila ya mpira.
Mbia alipost picha waliyopiga pamoja wakiwa timu ya taifa ya Cameroon
Taarifa za kifo cha Ekeng ambaye zilithibitishwa masaa mawili baada ya kufikishwa hospitali, zinakuja baada ya miaka 13 toka Cameroon impoteze kiungo wake Marc-Vivien Foe kwa stahili kama hiyo, tukio ambalo lilitokea June 26 2003 wakati wa michuano ya Kombe la mabara iliyokuwa inafanyika Ufaransa na mchezo ulikuwa dhidi ya Colombia.
Beki wa Arsenal Bellerin na mshambuliaji wa Man United Anthony Martial ni miongoni mwa mastaa walioguswa na kifo cha Ekeng
Ekeng alizaliwa March 26 1990 na amefariki akiwa na umri wa miaka 26 baada ya kuanguka uwanjani, Ekeng ndio alikuwa kaanza kupata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon ya wakubwa, muda mchache baada ya taarifa za kifo chake kuthibitika, mastaa wa soka walianza kupost na kuonesha huzuni kwa taarifa hizo.
No comments